Thursday, April 20, 2017

KUKAZA KUMPENDA MUNGU

Posted by Savior Ministry at 10:08 PM 0 CommentsZaburi 91:14-16
“Kwakua amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, kwa kuwa amenijua jina langu…”

Unaposema KUKAZA ni kinyume cha neno KULEGEA
Unapo KAZA kumpenda MUNGU maana yake unaongeza bidii kwaajili ya MUNGU, unaweka bidi kujifunza
Yeremia 48:10 Kufanya kazi kwa ULEGEVU ni Chanzo cha LAANA Ukilegea KUKAZA KUMPENDA BWANA unajitafutia LAANA.
NAMNA YA KUKAZA KUMPENDA MUNGU
KUKAZA tunamaanisha kuwa na JUHUDI za makusudi, kuwa na mipango na mikakati kabambe ili kumkaribia MUNGU aliye hai.
(wengi wameokoka lakini hawana juhudi za kumkaribia MUNGU baada ya kuwa umeokoka ni wakati wa wewe kuwa KARIBU na Mungu anasema nikaribieni mimi name nitawakaribia)
  •   KUSOMA NENO LA MUNGU
Unapokua unakaza KUMPENDA BWANA, kumbuka yeyote anaye nikaribia sitomtupa kamwe.
Umesumbuka mda mrefu, umeangaika mda mrefu lakini AMUA leo KUKAZA KUMPENDA MUNGU ili yeye aingilie kati katika maisha yako.
Panga Ratiba yako katika Kusoma NENO LA MUNGU, weka mipango ya KUONGEZA MAARIFA YA BWANA.
Lazima ukaze kutafuta NENO LA BWANA, biblia inasema siku zina kuja ambapo watu watatafuta NENO LA MUNGU na hawataliona

  • KUOMBA KWA BIDII
Lazima ujifunze kukaza kumpenda MUNGU katika SALA. 1 Petro 4:7 “mwisho wa Mambo  umekaribia basi iweni na aKili mkeshe katika sala”. Huu si wakati wa kuomba dakika Moja, ni wakati wa kukesha katika SALA.
Wakati mwingie si rahisi kuomba peke yako pata lifti kwa waombaji, jiunge kwenye vikundi vya maombi, nenda kwenye Mikesha, jinyime kula funga, hivi vitakusaidia kuwa karibu na MUNGU.
Acha kuomba kwasababu unataka kula, au kulala, au ili uponywe, unamwomba MUNGU ili aweze kuwa pamoja nawe njiani. KAZA KUMPENDA BWANA kuwa na bidii katika MAOMBI.

  •   USHUHUDA WAKO

Kaza kuwa na bidii katika ushuhuda wako, Daudi anasema wanao kutumaini wasiaibishwe kwaajili yangu eebwana wa majeshi. Wapo watu ambao hawapo makini na ushuhuda wa kwao, mtu anasema mtumishi wa Mungu, mimi ni muhubiri lakini matendo yake ni kinyume na kile anachokisema mtu huyu hawezi kukaza kumpenda MUNGU. Unapokaza kumpenda MUNGU ni lazima ushuhuda watu wanapo kutazama na kukuona wamuone MUNGU anaishi ndani yako, waone NGUVU ya Mungu inaishi ndani yako, waone Roho wa Bwana yuko ndani yako bila mashaka kabisa yaani watamani kuokolewa kwasababu ya maisha unayo yaishi. Wewe si wa ulimwengu huu wewe ni waulimwengu ujao unapokua kwenye nchi ya kwako unapaswa kuishi maisha ya nidhamu. Kaza katika kuwa na ushuhuda mzuri. Kuna mahali haupaswi kwenda au kushika maana vita haribu ushuhuda wako.
4.       KATIKA UAMINIFU WOTE (MTUMIKIE MUNGU KWA MALI ZAKO)
Mtumikie Bwana kwa mali yako, mali zako. Kwa habari ya fungu la kumi kaza kumpenda Bwana, acha visingizio kwa habari ya fungu la Kumi. Mtu mmoja alitoa mfano wa kutoa fungu la kumi eti alikua amebeba alafu kibaka akamuibia je atakua amesamehewa lile fungu la kumi? Labda tufikiri kwa style ingine je ulikua umebeba ada ya shule ya mwanao alafu ikaibiwa je utakua umesamehewa ada? Tumia nguvu zako kumtumikia Bwana. (Siku za Mwisho upendo wa wengi utapoa…) kumbuka tupo katika mashindano yeye ni Mungu wa wengi ukiringa ana watu wengi.


  •   KUTENDA KAZI YA MUNGU

Agizo kuu la Yesu ni kuihubiri injili, bilbia inasema enendeni ulimwengu wote kuihubiri Injili ya Bwana. Jirani zako, rafiki zako wote wanatamani kusikia habari za Yesu lakini wewe hauwaambii huko siyo kukaza Kumpenda MUNGU. Ukikaza kumpenda Mungu hata lugha yako inabadilika mara zote unafikiria habari ya Bwana.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUKAZA KUMPENDA MUNGU.
1.       Kaza katika Kujifunza na kusoma Neno lake.
2.       Kaza katika kuomba na kutafuta uso wa Bwana.
3.       Kaza katika kujenga ushuhuda mzuri mbele za Mungu na wanadamu
4.       Kaza katika uaminifu wote
5.       Kaza katika kutenda kazi ya Mungu kwa uaminifu.
FAIDA ZA KUKAZA KUMPENDA MUNGU
·         Mungu atakuokoka

Share This Post

Get Updates

Subscribe to our Mailing List. We'll never share your Email address.

0 comments:

The Savior Ministry Live Chat

© 2016 Savior Ministry.
Powered by Themes24x7 .
back to top