SAVIOR BIBLE SCHOOL

Shalom Shalom!
Karibu "Savior Bible School"
Savior Bible School imezaliwa na huduma ya Savior Ministry.
Savior Ministry ni huduma ambayo tupo kwaajili ya Ufalme wa Mungu na hasa ni "Macho yetu ya Tiwe NURU"  sawa na Waefeso 1:18

SAVIOR BIBLE SCHOOL LOGO: 
 
Savior Ministry our Objective:
" is to take ordinary people with ordinary backgrounds and introduce them to an Extraordinary Savior"
Ministry Motto:
"Bring Jesus into Reality"
Baada ya Kusema hayo napenda nikwambie,
Unapo amua kuwa sehemu ya Darasa hili unakua Mahali sahihi kabisa, na tuna Mshukuru Mungu kwaajili yako ya kwamba atakupatia Neema yakua miongoni mwa wanafunzi wa Shule hii.
Katika Darasa hii tutajifunza mengi sana sana. 
Lengo la Darasa hili ni:
Kukuweka katika VIWANGO vile Mungu anataka uwe.
Inawezekana Kabisa umekua kwenye wokovu mda mrefu napenda ujue Baada ya Darasa hili Utajiona kuwa Mtu wa Tofauti sana sana, na kuna mambo Utayaona Wazi wazi kwa Macho.
Hatutumii nguvu wala akili zetu, hii ni tumemuacha MUNGU mwenyewe achukue nafasi hii kwenye maisha yetu. Mithali 3:5-6
"Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;Katika njia zako zote mkiri yeye,Naye atayanyosha mapito yako."
Tutegemee nini toka SBS???
Yes, hili ni swali unaweza kuwa nalo. Tutegemee
Hayo yakisatokea sasa na ukikubalia
1. Kugeuzwa

2. Kufanywa Upya Nia yako.
na nayo Utaanza kuyajua hakika Mapenzi ya Mungu yaliyo mema.
  •  Utaishi Maisha ya Kumpendeza MUNGU.
  • Utakua Mkamilifu mbele za Mungu wako.
Sisi Savior Bible School tunasema wewe ni USHUHUDA WA MUNGU UNAE ISHI (Your the Living Testmony of Almighty God).
Warumi 12:2
"Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu."
Savior Bible School Verse: 
 2 Timotheo 2:15
"Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, UKITUMIA kwa HALALI NENO la KWELI ."
Anasema Ukitumia NENO LA KWELI lipi hilo NENO LA MUNGU
NENO hilo la KWELI ndilo KIOO CHETU na tutaishi hilo NENO LA MUNGU. ooh Haleluya!
Mungu Akubariki sana.
Hongera sana kwakua tunaimani utakua pamoja nasi kwa kujiunga na SBS
Nadhani sasa utakua umepata picha ya SBS ni nini?. 
Mode of Class
Darasa hili kutakua na Quiz, Assignment, na Test pia.  
Najua utaahangaa hili kwamba inawezekanaje? Sisi tunamuamini Mungu sana na kwake hakuna kisicho shindikana. 
Kwanini hizo zote.?
Najua pia utajiuliza hili, napenda ujue tunaposema Quiz, Assignment au Test tunajaribu kujua tunaenda wapi na hii ni Muhimu sana Mtu wa Mungu maana hapa itakusaidia sana sana kuwa Karibu na MUNGU wako wala hatufanyi hizi kwaajili yetu ni kwaajili yako na Ufalme. Nadhani nimeeleweka.
Baada ya Darasa hili, Utapata CHETI ya kwamba Umehitimu Savior Bible School. Na ni Muhimu sana ushiriki kwenye kila eneo maana kuna maksi zake na kama hautofanya Vizuri hautapata CHETI badala yake utapata BARUA ya kuonesha uliudhuria Darasa hili. Inaitwa Certificate of Attendance.
Mungu Akubariki sana. Hili Darasa ni Muhimu sana kwako.
Tunakupenda sana upo sehemu sahihi.
© TheSMT
SBS Coordinator
0762869876
0718418147
www.saviorministry.org

0 comments:

The Savior Ministry Live Chat

© 2016 Savior Ministry.
Powered by Themes24x7 .
back to top